Tuesday, March 1, 2011

TAARIFA YA MWANAMAPINDUZI KWA WAANDISHI WA HABARI

















Mch. Maximilian Machumu(mwenye suti nyekundu), akiwa na
Bw.Frederick Fussi- Afisa Mtendaji Mkuu-CEO wa RudishaMusic leo katika mkutano na waandishi wa habari.

Awali ya yote, kwa niaba ya Kampuni yetu ya UFUFUO NA UZIMA MUSIC LTD, kupitia programu yetu ya RudishaMusic napenda kuchukua fursa hii kwa namna ya pekee kabisa, kukushukuru kwa kukubali wito wetu na kuamua kuja katika mkutano huu.

RudishaMusic ni programu mpya iliyochini ya Kampuni yetu yenye lengo la kurudisha hadhi ya Muziki wa Injili hapa nchini, kwa maana ya kwamba kuinua vipato vya waimbaji wa Muziki wa injili hapa nchini, kujenga na kuongeza uwezo wa waimbaji wa muziki wa injili kuwafikia maelfu ya watu kwa urahisi.

RudishaMusic kwa mara ya kwanza kabisa hapa Tanzania, ikishirikiana na Mwanamuziki wa Muziki wa injili, Mch. Maximilian Machumu akiwa na bendi yake inayofahamika kwa jina la Mwanamapinduzi Band, wanatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yao ya kwanza inayofahamika kwa jina la Bonde la Kukata Maneno. Uzinduzi huu utafanyika siku ya tarehe 6 Machi 2011 katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa 7 mchana.

Moja kati ya malengo la Tamasha hili ni kufanya uzinduzi wa Albamu ya Bonde la Kukata Maneno na kuiweka wakfu kwa Mungu. Albamu hii ina jumla ya nyimbo nane na inapatikana katika Mfumo wa DVD, VCD, na Tape.

Mwanamapinduzi Band, inaongozwa na Mch. Maxiliam Machumu akiwa na jumla ya waimbaji wanne ambao ni Mary Maximilian, Saraphina Urio, Chatherine Patrick na Veraikunda Urio

Lengo kuu la uzinduzi huu ni kusaidia ujenzi wa kituo cha watoto yatima maeneo ya Kiluvya. Sehemu ya mapato ya uzinduzi ikiwa ni pamoja na mnada wa DVD, VCD na Tape imekusudiwa kutumika katika kusaidia ujenzi huo. Makadirio ya Ujenzi wa kituo hicho ni takribani Tshs. 120,000,000 milioni.

Mgeni rasmi katika Tamasha hili, atakuwa Waziri Mkuu Mstafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Edward Lowassa. Mgeni Rasmi katika Tamasha hili anatarajiwa kutumia fursa hii kuzindua Albamu ya Bonde la Kukata Maneno katika mfumo wa DVD, VCD na Tape.

Tamasha litapambwa na waimbaji mbalimbali wa Muziki wa Injili ambao wanafanya vizuri sana katika medani ya Muziki huu. Waimbaji hao ni Ambwene Mwasongwe, Martha Mwaipaja, John Lisu, Jackson Benty, Mch.Stephen Wambura na wengine wengi.

Tamasha hili limepata udhamini kutoka kwa makampuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Chinese Restaurant ambao ni wadhamini wakuu, wakishirikiana na wadhamini washirika ambao ni ABE Professional Sound, Neden Designers Group na WAPO Radio FM.

Mwisho kabisa nitumie fursa hii kuwakaribisha wapenzi na mashabiki wa Muziki wa Injili hapa nchini katika Tamasha hili

Taarifa hii imetolewa na:-

Afisa Mtendaji Mkuu leo asubuhi katika mghahawa wa Chinise Restaurant alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia uzinduzi huo.