Monday, March 7, 2011

LOWASA ACHANGIA MILIONI 10 KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU YA BONDE LA KUKATA MANENO

Waziri Mkuu Mstaafu (MB) Mhe. Edward Lowasa akizindua rasmi albamu ya Muimbaji wa Muziki wa Injili Mchungaji Maximilian Machumu a.k.a Mwanamapinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Dimond Jubilee leo, kulia ni Maximilian Machumu na Katikati ni Askofu Gwajima

Tamasha hilo ambalo limeambatana na mahubiri kutoka kwa Askofu Gwajima limeshirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili hapa nchini akiwemo John Lisu, Jackson Benti, Ambwene Mwasongewe, Martha Mwaipaja, huku waimbaji wapya wa muziki wa injili na Mbunge wa viti maalumu Mh. Vick Kamata akitambulisha wimbo wake mpya wa Injili na kukonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wa muziki wa Injili.
Katika uzinduzi huo Mgeni rasmi Mh. Lowasa akishuhudia kupiga tafu kuchangia ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima kwa kutoa Shilingi Milioni 10.
Muimbaji Maximilian Machumu akiimba katika Uzinduzi wa Albamu yake ya Kwanza inayofahamika kama Bonde la Kukata maneno. Kushoto ni mkewe Bi. Mary Maximilian na kulia kwake ni Veraikunda Urio, na Catherine Patrick
Askofu Gwajima akiomba maombi maalumu ya Kufungua uzinduzi wa Albamu ya Bonde la Kukata Maneno ya Mwanamapinduzi Mch. Maximilian Machumu. Pembeni ni Rita Chiwalo. mtangazaji wa WAPO radio Fm ambaye pia alikuwa MC katika Tamasha hilo.
Muimbaji wa nyimbo za Injili ambaye pia ni Mbunge wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Vick Kamata akiimba huku akiigiza kutubu mbele ya Mfalme, Mchungaji Machumu Maximilian wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Bonde la Kukata maneno chini ya Mwanamapinduzi Band inayoongozwa na Machumu Maximilian
Mh. Vick kamata akitambulisha rasmi wimbo wake mpya katika medani ya muziki wa Injili, wimbo unasema "Sitaki kuku nataka msamaha" leo katika Ukumbi wa Dimond Jubilee
Muimbaji Ambwene Mwasongwe akiimba katika albamu ya Bonde la kukata maneno ya Maximilian Machumu
Umati mkubwa Dimond Jubilee katika Uzinduzi wa Albamu ya Bonde la Kukata Maneno ya Mwanamapinduzi Band