Sunday, December 19, 2010
Monday, December 6, 2010
K-Basil Aiga rasmi kambi ya makapera!
Mwanamuziki wa muziki wa injili Kashumba Basil (K-Basil) jana ameiga rasmi kambi ya makapera baada ya kuamua kuvunja ukimya na kujitwalia mke.
K-Basil alifunga pingu za maisha siku ya jumapili majira ya saa 9 alasiri katika kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kama Ufufuo na Uzima ambapo ndoa yao ilifungwa chini ya Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Mch. Josephat Gwajima na kuafutiwa na maombi maalumu ya wachungaji kutoka Japani ambao waliibariki ndoa hiyo.
Sherehe ya kukata na shoka ya kuwapongeza maharusi hao ilifanyika kuanzia saa moja usiku katika ukumbi wa Kilimanjaro Park uliopo Sinza jijini Dar es Salaam.
RudishaMusic inawatakia maisha mema na yenye baraka katika ndoa yenu.

Saturday, November 20, 2010
Breaking News: K-Basil mbioni kujitwalia Jiko

Mwimbaji wa muziki wa Injili Kashumba Basili (K-Basil) aliyewahi kutamba katika medani ya muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) kama unayoitwa na vijana wengi wa kileo ambaye ameokoka tangu mwaka 2007 anatarajia kufunga pingu za maisha hivi karibuni.
RudishaMusic ilihabarishwa na mwanamuziki huyu kuwa ndoa yake itafungwa tarehe 5 Disemba 2010. RudishaMusic itakuletea habari moto moto kuhusiana na uimbaji wa muziki wa injili wa K-Basil sambamba na matukio ya ndoa yake hivi karibuni.
Thursday, October 14, 2010
Saraphina Urio

Je unafahamu kuwa Dada huyu unayemuona hapa ni muimbaji mahiri wa Muziki wa injili? Endelea kufuatilia RudishaMusic. Saraphina kama mmoja wa "Viriba vipyaa" chenye "Divai mpyaa" atakuja hivi karibuni na albamu yake mpyaa. Tayari wimbo wake uitwao "Sifa zivume" Umeanza kutamba kwa kupigwa mara kadhaa wa kadha katika kituo cha WAPO RADIO katika kipindi cha "zilizotufikia" hapa jijini Dar es Salaam. Saraphina Urio is Coming Soon only at RudishaMusic.
Unataka Kumjua Barnabas zaidi?
Monday, October 11, 2010
Rachel Marlon: Nipo Mbioni kutoa albamu yangu mpyaaa
RudishaMusic imefanya mahojiano na mwanamuziki Rachel Marlon na kutaka kudodosa nini hasa kinaendelea juu ya mipango yake ya kimuziki na haya ndio aliyoyaelezea. "Nipo mbioni kutoa Albamu yangu mpya itakayokwenda kwa jina la SINA HOFU TENA. Albamu hii itachukua muda wa miezi kama mitatu hivi kuwa mtaani kuanzia sasa. Vilevile nafikiria kurekodi video ya hii albamu yangu."
Haya wapenzi wa muziki wa injili kaeni mkao wa kula na kupata ladha mpyaa kutoka kwa dada yetu Rachel Marlon. Albamu yake inarekodiwa katika studio yake mwenyewe. RudishaMusic itaendelea kukujuza juu ya ujio ya albamu hii pindi itakapotoka.
Friday, October 8, 2010
Christina Shusho
Subscribe to:
Posts (Atom)