Monday, September 20, 2010

Jane Misso azindua albamu yake "Uinuliwe"

Saa chache kabla ya kufanya uzinduzi wa albamu yake, Jane Misso alipiga show kali ya kumtukuza YEHOVA katika viwanja vya Tanganyika packers, ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima iliyopo Kawe jijini Dar es salaam.
.
Jane Misso kama anavyoonekana hapa akimwaibisha shetani kwa kumnyima sifa kwa kibao chake maarufu "Umoyo" Huku akiimba kwa furaha na kumpatia sifa YEHOVA.
Jane Misso akipiga show yake huku maelfu ya watu wakiimba pamoja naye. Muimbaji huyu alizindua albamu yake siku ya Jumapili, 19 Agosti 2010 katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Albamu yake mpya inakwenda kwa jina la "Uinuliwe".

Picha zote kwa hisani ya Ufufuo na Uzima.

Peace Muluu amsindikiza Jane Misso katika Uzinduzi wa albamu yake

Peace Muluu kutoka Nairobi Kenya, muimbaji wa nyimbo za injili
ambaye alishambulia jukwaa pamoja na Jane Misso. Katika picha Muluu akiimba ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima.


Peace Muluu akiimba ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima, iliyopo kawe jijini Dar es salaam, katika viwanja vya Tanganyika Packers.

Picha zote kwa hisani ya Ufufuo na Uzima.

Thursday, September 16, 2010

Wednesday, August 11, 2010

Rachel Marlon akitumbuiza!


Mwanamuzi Rachel Marlon anayetamba na kibao chake kiitwacho"Sina hofu tena" akiimba na kucheza huku pembeni yake akisindikizwa na Kashumba Basil.

Wanamuziki wa Injili kutoka Japan


wanamuziki wa muziki wa Injili Kutoka Japan wakiimba kama walivyobambwa na kamera zetu ndani ya Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church almaarufu kama Nyumba ya ufufuo na Uzima iliyopo kawe jijini Dar es Salaam.

Sunday, August 1, 2010

City Christian Center wafanya tamasha la Uzalendo la vijana

City Christian Center , Upanga wamefanikiwa kufanya bonge la tamasha la Uzalendo likiwalenga vijana wa Kitanzania waishio jijini Dar es salaam. Tamasha hilo lilifanyika siku ya jumamosi 31 Julai 2010 katika ukumbi wa City Christian Centre, upanga.

Tamasha hili la muziki wa injili lilipambwa na waimbaji na wanamuziki mahiri wa muziki wa injili kutoka DPC (Dar es Salaam Pentecostal Church) na CCC (City Christian Centre). Waimbaji wa kikundi cha “The next level” kutoka CCC waliporomosha muziki wa sifa na kuabudu ambapo vijana walioshiriki tamasha hilo walipata fursa ya kucheza na kumwimbia BWANA YESU kwa shangwe isiyokifani.

Mmoja kati ya wanamuziki maarufu hapa nchini John Lisu alikuwepo ndani ya tamasha hili na kukipiga kibao cha muziki maarufu kama “Yakobo” huku alikilitwanga gitaa lake kwa umahiri mkubwa .