Sunday, August 1, 2010

City Christian Center wafanya tamasha la Uzalendo la vijana

City Christian Center , Upanga wamefanikiwa kufanya bonge la tamasha la Uzalendo likiwalenga vijana wa Kitanzania waishio jijini Dar es salaam. Tamasha hilo lilifanyika siku ya jumamosi 31 Julai 2010 katika ukumbi wa City Christian Centre, upanga.

Tamasha hili la muziki wa injili lilipambwa na waimbaji na wanamuziki mahiri wa muziki wa injili kutoka DPC (Dar es Salaam Pentecostal Church) na CCC (City Christian Centre). Waimbaji wa kikundi cha “The next level” kutoka CCC waliporomosha muziki wa sifa na kuabudu ambapo vijana walioshiriki tamasha hilo walipata fursa ya kucheza na kumwimbia BWANA YESU kwa shangwe isiyokifani.

Mmoja kati ya wanamuziki maarufu hapa nchini John Lisu alikuwepo ndani ya tamasha hili na kukipiga kibao cha muziki maarufu kama “Yakobo” huku alikilitwanga gitaa lake kwa umahiri mkubwa .