Friday, December 31, 2010

Happy New Year 2011

Happy New Year all Tanzanians.......... Happy New Year all Tanzanians and the world as the whole....
Hua huyu ni ishara ya Roho Mtakatifu.....RudishaMusic inawaombea vijana wote wanaomwimbia Mungu katika muziki wa Injili wajazwe Roho Mtakatifu na Wapae juu kama tai katika huduma yao ya uimbaji katika mwaka huu 2011. Wamngojao BWANA watapata nguvu mpyaa nao watapaa juu kama tai...

Taswira Mpyaa na Mwaka Mpyaaa 2011

Hapa katika Picha John Lissu akiwa DPC-Dar es Salaam Pentecostal Church, Kinondoni akicharaza gitaa lake...

Moja kati ya wanamuziki wachache nchini katika medani ya muziki wa Injili ambao wanapoimba muziki wao ni wa tofauti na unaambana na upako katika nyimbo za kusifu na Kuabudu ni John Lissu. Mwaka 2011 Rudisha Music itakuletea series ya matukio yanayomuhusu Lisu katika huduma ya Uimbaji ambayo Mungu amempa ili amtumikie Yeye.
Tunapoingia mwaka Mpya RudishaMusic imejipanga kukujuza juu wa vijana wengi wanoimba na kucheza kwa ajili ya Utukufu wa Jina la BWANA. Vijana hawa pichani wanaitwa Shekhinah Dancers ni vijana mahiri sana kutoka TAG-City Christian Centre-CCC Upanga.

Picha zote kwa hisani kubwa ya The Next Level-CCC, Upanga, Dar es Salaam