RudishaMusic imefanya mahojiano na mwanamuziki Rachel Marlon na kutaka kudodosa nini hasa kinaendelea juu ya mipango yake ya kimuziki na haya ndio aliyoyaelezea. "Nipo mbioni kutoa Albamu yangu mpya itakayokwenda kwa jina la SINA HOFU TENA. Albamu hii itachukua muda wa miezi kama mitatu hivi kuwa mtaani kuanzia sasa. Vilevile nafikiria kurekodi video ya hii albamu yangu."
Haya wapenzi wa muziki wa injili kaeni mkao wa kula na kupata ladha mpyaa kutoka kwa dada yetu Rachel Marlon. Albamu yake inarekodiwa katika studio yake mwenyewe. RudishaMusic itaendelea kukujuza juu ya ujio ya albamu hii pindi itakapotoka.