Saturday, November 20, 2010

Breaking News: K-Basil mbioni kujitwalia Jiko


Mwimbaji wa muziki wa Injili Kashumba Basili (K-Basil) aliyewahi kutamba katika medani ya muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) kama unayoitwa na vijana wengi wa kileo ambaye ameokoka tangu mwaka 2007 anatarajia kufunga pingu za maisha hivi karibuni.

RudishaMusic ilihabarishwa na mwanamuziki huyu kuwa ndoa yake itafungwa tarehe 5 Disemba 2010. RudishaMusic itakuletea habari moto moto kuhusiana na uimbaji wa muziki wa injili wa K-Basil sambamba na matukio ya ndoa yake hivi karibuni.