Mwanamuziki wa muziki wa injili Kashumba Basil (K-Basil) jana ameiga rasmi kambi ya makapera baada ya kuamua kuvunja ukimya na kujitwalia mke.
K-Basil alifunga pingu za maisha siku ya jumapili majira ya saa 9 alasiri katika kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kama Ufufuo na Uzima ambapo ndoa yao ilifungwa chini ya Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Mch. Josephat Gwajima na kuafutiwa na maombi maalumu ya wachungaji kutoka Japani ambao waliibariki ndoa hiyo.
Sherehe ya kukata na shoka ya kuwapongeza maharusi hao ilifanyika kuanzia saa moja usiku katika ukumbi wa Kilimanjaro Park uliopo Sinza jijini Dar es Salaam.
RudishaMusic inawatakia maisha mema na yenye baraka katika ndoa yenu.